Naibu Waziri Wizara Ya Afya Mhe: Dkt Faustine Ndungulile Afanya Ziara Hospitali Ya Rufaa Ya Mkoa Wa Iringa.

image description

Wednesday 1st, February 2023
@Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa

Mnamo tarehe 06-01-2020 majira ya saa 4 asubuhi mhe Naibu waziri alifanya ziara katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa iringa akiongozana na timu yake nzima kutoka wizarani .

Katika ziara hiyo mhe naibu waziri alianza kwa kukagua vitengo mbali mbali vya kutolea huduma hospitalini hapo ambapo vitengo hivyo ni Bima, wagonjwa wa nje, sehemu ya mapumziko ya ndugu wa wagonjwa, idara ya meno, idara ya watoto, idara ya kina mama na uzazi, maabara, famasi, na kisha kufanya mazungumzo na wakuu wa idara na vitengo wa hospitali.