HUDUMA ZA DIALYSIS

Posted on: February 10th, 2022

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa imezindua huduma ya kusafisha damu inayojulikana kama DIALYSIS,ambapo tayari wagonjwa wameanza kupata huduma hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa IRINGA Mh QUEEN SENDIGA ametembelea mradi huo na kujionea namna huduma inavyofanya kazi,na amepongeza uongozi wa Hospitali ya RUFAA na kuutaka uongozi kuutunza mradi huo ili wananchi waweze kupata huduma hiyo kwa karibu.

Kabla ya kuzinduliwa huduma hiyo wagonjwa walikuwa wakienda kutibiwa DODOMA,lakini kwasasa wataweza kupata huduma hiyo katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.