WIKI YA AFYA YA KINYWA NA MENO KUANZIA TAREHE 14/03 MPAKA TAREHE 20/03/2022

Posted on: March 15th, 2022

Wiki hii kuanzia tarehe 14/03 mpaka tarehe 20/03/2022 ni wiki ya Afya ya Kinywa na Meno na kitaifa itafanyika mkoani Songea.

Dr Atupele Mwandiga amesema ni muhimu wananchi kufanya kufanya uchunguzi wa Afya ya Kinywa na Meno angalau mara mbili kwa mwaka ili kujiepusha na magonjwa ambayo chanzo chake ni  Kinywa na Meno.

Dr amesema mgonjwa wa Kinywa na Meno yupo katika hatari ya kupata magonjwa kama matatizo ya Figo, ugonjwa wa Kansa lakini kwa mwanamke yupo katika hatari ya kujifungua mtoto ntiti au mwenye uzito mdogo.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni 'JIVUNIE KINYWA CHAKO KWA USTAWI WA AFYA YAKO'

Amewataka wananchi kujitokeza katika hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa ili waweze kufanyiwa uchunguzi